Monday, December 30, 2019


GERSON Fraga,raia wa Brazil, kiungo mkabaji wa Simba amesema kuwa siri kubwa ya kufanya vema inabebwa na ushirikiano ulio ndani ya kikosi cha Simba pamoja na mashabiki wake kiujumla.

Fraga ana bao moja kwenye Ligi Kuu Bara alilofunga mbele ya KMC kwenye ushindi wa mabao 2-0 mechi iliyochezwa Uwanja wa Uhuru akimalizia pasi ya Francis Kahata.

Akizungumza na Saleh Jembe, Fraga amesema kuwa anafurahi kuwa ndani ya Simba pamoja na kuwa miongoni mwa familia ya watanzania wenye upendo.

"Ni nchi yenya amani utulivu na upendo, kikubwa kinachotufanya tuwe bora na kufanikiwa ni ushirikiano uliopo ndani ya Simba," amesema.

Simba imefunga jumla ya mabao 25 kwenye jumla ya mechi 12 ilizocheza inaongoza ligi ikiwa na pointi 31.

0 comments:

Post a Comment