SAKATA la mchezaji, Ditram Nchimbi aliyesajiliwa ndani ya Yanga akitokea Polisi Tanzania limezua suara mpya baada ya Polisi Tanzanie kuendelea kumkomalia mchezaji huyo.
Polisi Tanzania walimchukua Nchimbi kwa mkopo wa mwaka mmoja kutoka Azam FC na kwa sasa amesajiliwa na Yanga baada ya kufikia makubaliano na Azam FC na kuweka mzigo mezani wa milioni 40.
Mabosi zake wa zamani Polisi Tanzania inaelezwa kuwa hawajakubaliana na dili la Nchimbi kutimkia ndani ya Yanga kwani bado makubaliano yao na Azam hayajatimizwa.
Polisi Tanzania wanadai kuwa mkataba wao upo kwenye Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) jambo linalowapa kiburi kwa mchezaji huyo mwenye mabao manne ndani ya Ligi Kuu Bara.
Inaelezwa kuwa Polisi Tanzania wanahitaji kulipwa gharama za mchezaji huyo ambaye ameanza mazoezi ndani ya Yanga na uongozi wa Yanga inaelezwa kuwa upo kwenye mchakato wa kumalizana na Polisi Tanzania ili kumtumia kwenye mchezo wao dhidi ya Simba, Januari, 4,2020.
0 comments:
Post a Comment