Monday, December 30, 2019



Simba imethibitisha kuwa uwanja wao wa Mo Simba Arena, uliopo Bunju utaanza kutumika kwenye michuano ya ligi kuu ya soka ya wanawake Tanzania Bara.

Taarifa ya klabu hiyo imeeleza kuwa mchezo wa leo kati ya timu ya Simba Queens dhidi ya Kigoma Sisters utapigwa Mo Simba Arena.

'Timu ya Simba Queens leo inacheza mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake dhidi ya Kigoma Sisters. Mchezo huo unapigwa kwenye uwanja wa Mo Simba Arena kuanzia saa 10:00 jioni', imeeleza taarifa hiyo.

Ikumbukwe Uwanja wa Mo Simba Arena wenye viwanja viwili ambavyo pia vinatumika na timu ya wanaume ya Simba kufanyia mazoezi, ulipokelewa na klabu pamoja na mashabiki kutoka kwa mkandarasi Desemba 7, 2019.

0 comments:

Post a Comment