Monday, December 30, 2019



Klabu ya Borussia Dortmund imemsajili mshambuliaji Erling Braut Håland kutoka Salzburg kwa mkataba utakaoisha 2024.

Kinda huyo wa Norway mwenye umri wa miaka 19, awali alikuwa akiripotiwa kuwindwa na Manchester United ya nchini England.

Haaland ambaye amefunga magoli nane katika michuano ya klabu bingwa Ulaya msimu huu, anatua Dortmund kwa ada ya pauni milioni 18 na anaripotiwa kuwa atakuwa akilipwa mshahara wa Pauni 130,000 kwa wiki.

0 comments:

Post a Comment