Mazungumzo ya Chelsea kuhusu mkataba
mpya wa mshambuliaji wa England Tammy Abraham yamekwama kwa sababu
kiungo huyo wa miaka 22-anataka kulilipwa - £180,000 kwa wiki - sawa na
winga Callum Hudson-Odoi, 19. (Goal)
Mkufunzi wa Liverpool Jurgen
Klopp amekubali kumpoteza kiungo wa kati wa England Adam Lallana, 31,
mwisho wa msimu huu. (Telegraph)Kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, 26, amekiri kuwa Manchester United haitamuuza mwezi Januari. (Sky Sports, via Metro)
Beki wa Argentina Marcos Rojo, 29, anajiandaa kuondoka Manchester United mwezi Januari wakati wa dirisha la uhamisho wa wachezaji litakapofunguliwa. (Manchester Evening News)
Thierry Henry atakuwa mmoja wa watakaowania nafasi ya ukufunzi wa Barcelona ikiwa mkufunzi wa sasa Ernesto Valverde ataondoka klabu hiyo mwaka 2020. (Sport - in Spanish)
Mkufunzi mpya wa Arsenal Mikel Arteta anakabiliwa na kibarua kigumu kumshawishi mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 30, kusalia katika klabu hiyo badaa ya msimu huu utakapokamilia. (Telegraph)
Everton wanaongoza kinyang'anyiro cha usajili wa winga wa Colombia James Rodriguez, 28, kutoka Real Madrid. (El Desmarque - in Spanish)
Fiorentina inataka kumsaini mshambuliaji wa Wolverhampton na Italia Patrick Cutrone, 21, kwa mkopo hadi mwisho wa msimu. (Gazzetta dello Sport - in Italian)
Aston Villa inataka kumsajili kiungo wakati wa Chelsea Danny Drinkwater, 29, kwa mkopo mwezi Januari January. Mchezaji huyo wa England kwa sasa yuko Burnley kwa mkopo. (Sky Sport
0 comments:
Post a Comment