Bondia Abdallah
Pazi ‘Dullah Mbabe’ bingwa wa Super Middle WBO Asian Pacific alioutwaa 2019 kwa
kumtwanga kwa TKO, Zulipikaer Maimaitiali raia wa China katika raundi ya tatu,
amesema kuwa msosi wake mkubwa mchana ni ugali na asubuhi anapenda chai na
chapati tatu.
Akizungumza na
Kijiwe cha Ndondi, Mbabe alisema kuwa katika vitu ambavyo anapenda kuzingatia
japo Kibongobongo ni ngumu ni masuala ya msosi hasa kutokana na mazoezi
anayofanya.
“Asubuhi napenda
nikipata chai na chapati tatu nakuwa
fresh na mchana mimi ugali huniambii kitu
napenda kinoma
na huwa nakula kweli sio kibishoo,” alisema Mbabe.
0 comments:
Post a Comment