KUTOKANA na timu ya Simba iliyo chini ya Kocha Mkuu, Sven Vanderbroeck kumrejesha ndani ya kikosi hicho mchezaji wao wa zamani, Shiza Kichuya, Saleh Jembe amekuwa na maswali matano ambayo anahitaji msaada kujibiwa.
Jembe amesema: "Kama umeelewa vizuri TUSAIDIANE.... Sijawahi kusema Shiza Kichuya ni mchezaji mbaya lakini nilikuwa najiuliza maswali kadhaa, kama una majibu TUSAIDIANE, ndio uanamichezo wenyewe... SIMBA KUMSAJILI KICHUYA NI KWA SABABU YA.... 1. Kuwahi Yanga wasimpate...
2. Siasa ya kupoza Sakata la bosi...
3. Kumsitiri kijana wao baada ya mambo kutoenda poa..
4. Usajili wa Simba una walakini kwa namba za pembeni
5. Kweli ni chaguo la Kocha au Nani anaamua... ....????
0 comments:
Post a Comment