Thursday, January 16, 2020


 


UONGOZI wa Singida United umesema kuwa utapambana msimu huu kubaki ndani ya ligi kutokana na usajili walioufanya.

Singida United haijawa na msimu mzuri kutokana na kutokuwa na matokeo mazuri imeshinda mechi mbili tu mpaka sasa za ligi kuu jambo ambalo limewashtua viongozi kufanya kikao na wachezaji.

Akizungumza na Saleh Jembe Ofisa Habari wa Singida United, Cales Katemana amesema kuwa wachezaji walikuwa na masuala mengi yaliyokuwa yanawasumbua kikao walichofanya kitawasaidia kurudi kwenye morali.

"Mambo hayakuwa mazuri mwanzo ila tayari kwa sasa tumeanza kurejea kwenye ubora wetu, ushindi mbele ya Ruvu Shooting umetuongezea nguvu wale wanaofikiria tutashuka daraja hilo litabaki kuwa stori," amesema. 

Singida United imefanya usajili wa wachezaji wakongwe ambao wameanza kazi ikiwa ni pamoja na Haruna Moshi 'Boban' na Athuman Idd Chuji.

0 comments:

Post a Comment