MICAH Richard, mchezaji wa zamani wa Manchester City amesema kuwa mfumo alioutumia Kocha Mkuu wa City, Pep Guardiola ulimponza mbele ya Manchester United na kukubali kufungwa bao 1-0 mbele ya Manchester United.
Usiku
wa Jumatano,Januari 29, City ilikubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa
wapinzani wao wakubwa Manchester United na bao pekee la ushindi
lilifungwa na Nemanja Matic aliyefunga bao pekee kwenye mchezo huo
dakika ya 35 na alitolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 76.
Licha
ya ushindi huo, United haitasonga mbele kwenye fainali kwa kuwa
ilipoteza mchezo wa kwanza kwa kufungwa mabao 3-0 na kufanya itolewe kwa
jumla ya mabao 3-2.
"Guardiola
alikuwa anafikiria sana mechi yake na akashindwa kuzuia hisia zake
jambo lililomfanya hata ashindwe kupanga kikosi kwa umakini akiwa na
wachezaji wake ndani ya Uwanja wa Etihad.
"Jambo
hilo liliwapa nafasi United kucheza kwa kujiamini na kufanya makubwa
ambayo yaliwapa matokeo na ingekuwa hivyo mpaka mwisho basi habari
ingekuwa nyingine," amesema.
0 comments:
Post a Comment