Bocco amesema kuwa wanatambua kazi kubwa waliyonayo ni kutafuta ushindi jambo ambalo watalifanya siku zote.
Kwenye
ushindi wa mabao 3-1 aliyopata Simba mbele ya Zimamoto, Bocco naye
alitupia bao moja huku mengine yakifungwa na Sharaf pamoja na Ibrahim
Ajibu.
"Mashabiki
wanahitaji kuona timu inapata matokeo chanya, tupo vizuri na
tunaendelea kupambana kwa ajili ya kufikia malengo na mafanikio,
tunaamini tutapata kile ambacho tunakihitaji.
"Ushindani ni mkubwa na kila timu inahitaji matokeo tutakachofanya ni kujituma ndani ya uwanja," amesema Bocco.
Siba itamenyana na Azam FC kwenye mchezo wa nusu fainali unaotarajiwa kuchezwa Ijumaa, Januari 10uwanja wa Gombani
0 comments:
Post a Comment