WAKATI
Ligi Kuu England msimu wa 2019/20 ikiwa ndio mbichi kabisa, Teemu Pukki
wa Norwich alionekana ameibuka na mapinduzi mapya.
Alikuwa
akifunga mfululizo na kuwafanya wengi kuamini angeshika nafasi hiyo ya
waliofunga mabao mengi kwa muda mrefu. Lakini sasa yuko katika nafasi ya
10 akiwa na mabao tisa.
Ilionekana
kama Sergio Aguero na mwenzake Harry Kane ambao hushindana mara nyingi
wangeibuka na kumkamata Pukki na ikiwezekana kuongoza, sasa wako katika
nafasi ya sita kwa Kane mwenye mabao 11 na nane kwa Aguero akiwa na
mabao 10.
Ligi
bado inaendelea na kuna uwezekano mambo yakabadilika na ambaye bado
yuko chini akaibuka na kufunga mabao mengi na kushika nafasi ya juu
kabisa.
Hata
hivyo, katika Premier League, hakuna zawadi ya mabao, badala yake
mshambuliaji analazimika kufanya kazi hasa ili kupata bao moja au
mawili.
Kinachoonekana
ni kitu tofauti sana na kilichokuwa kikitokea katika EPL misimu
mingine. Kwa wanaoongoza msimu wote walio katika tatu bora, mabao yao
mengi wamefunga zaidi ugenini.
Yaani
washambuliaji hao, wamekuwa bora zaidi na timu zao wanapokuwa na timu
za ugenini, jambo ambalo ni tofauti kidogo kwa Pukki, Aguerro na Kane
ambao wamekuwa bora zaidi wanapokuwa katika viwanja vyao vya nyumbani.
Katika
mabao yake 11, Kane amefunga sita akiwa nyumbani na matano ugenini.
Aguero kafunga 10, kati ya hayo sita nyumbani na manne ugenini na Pukki
ana tisa, sita akiwa amefunga nyumbani na matatu ugenini.
Hapa
unawaona wale walio juu, Jamie Vardy wa Leicester City ambaye aliibuka
baadaye kama kimondo ana mabao 17 kileleni mwa wafungaji wanaochuana
vikali na kati ya hayo, nane amefunga kwenye Uwanja wa nyumbani wa Kings
Power na tisa amefunga akiwa ugenini.
Nafasi
ya pili hadi sasa inashikiliwa na Pierre-Emerick Aubameyang ambaye
amefunga mabao 13, kati ya hayo matano ndio yamepatikana nyumbani
Emirates na nane amefunga katika mechi za ugenini kama ilivyo kwa Tammy
Abraham wa Chelsea ambaye amefunga mabao manne tu pale Stamford Bridge
na nane akiwa ugenini, kama unakumbuka bao la nane amelifunga akiwa
Emirates, Chelsea ikiizamisha Arsenal na kumfanya afikishe mabao 12.
Mabao ni mabao tu, yanahesabika katika idadi ya wafungaji. Lakini inajulikana namna kunavyokuwa na ugumu wa kufunga ugenini.
Timu
nyingi zinapokuwa katika viwanja vya nyumbani zinakuwa ngumu sana.
Zinapambana kuhakikisha zinashinda na hata aina ya uchezaji inakuwa
tofauti kidogo, wenyeji ndio wanakuwa wanasukuma mashambulizi mengi
zaidi hivyo kuwafanya wageni wajilinde au kuwa na mashambulizi machache.
Mwendo
wa kuonekana wanaoongoza wamefunga ugenini zaidi maana yake, wafungaji
wametoa adhabu wakiwa katika viwanja mbali na nyumbani kwao. Hii maana
yake kuna kitu kinabadilika katika soka la England na ikiwezekana
mifumo.
Kwamba
timu zinapokwenda viwanja vya ugenini, zina nafasi ya kupata mabao
zaidi kupitia mfumo wa kufunga wa timu nyingi zinapokuwa katika viwanja
vya nyumbani kwa kuwa zaidi zinalazimika kutaka kuwafurahisha mashabiki
wao lakini hii inakuwa ni hatari zaidi kwao.
Vardy
anaonekana pia ni hatari zaidi kuanzia dakika ya 61 hadi 75 kwa kuwa
katika muda huo amefunga mabao matano. Hali kadhalika Aubameyang
amefunga mabao manne katika muda huo kati ya 13 aliyofunga.
Upande
wa Abraham, anaonyesha hatari wakati wowote na hasa kuanzia dakika ya
16 hadi 30 na 31 hadi 45 ambazo amefunga mabao matatu kwa kila kipindi,
maana yake sita.
Bado
kuna nafasi kwa kina Aguero na Kane, kwa kuwa nafasi ya kufunga wanayo
lakini hii inaonyesha lazima wabadilike, kama milango bado si rafiki
sana wanapokuwa wanacheza nyumbani, basi waongeze nguvu ya kuwa msaada
katika timu zao kwa mechi za ugenini.
0 comments:
Post a Comment