KOCHA
Mkuu wa Yanga, Luc Eymael raia wa Ubelgiji amefunguka kuwa ana uhakika
mkubwa wa timu yake kuweza kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu bara msimu huu
kutokana na kuonekana kwa mabadiliko kwenye kikosi chake.
Kabla
ya matokeo ya jana, Yanga ilikuwa imepitwa pointi 16 na vinara Simba
ambao wana alama 50 wakati wao Yanga wanazo 34 wakiwa nafasi ya tatu.
Eymael
alisema: “Kikubwa ambacho nakiona, ni kwamba timu yangu imebadilika kwa
kiwango kikubwa na kadiri siku zinavyokwenda ndiyo inazidi kuwa bora,
naamini nafasi ya ubingwa tunayo tena kubwa.
“Binafsi
sina presha juu ya hilo na wala hatupaswi kuogopa kwamba nani anaongoza
ligi kwa lengo la kukata tamaa, jambo kubwa ni kuendelea kupigana kuona
kwanza tunawapita wapinzani wetu ili kuweza kufikia ubingwa kitu
ambacho bado kipo kwenye uwezo wetu.”

0 comments:
Post a Comment