Mshambuliaji
Mbelgiji, Romelu Lukaku akishangilia baada ya kuifungia Inter Milan bao
la nne dakika ya 90 na ushei ikitoka nyuma na kuichapa AC Milan 4-2
usiku wa jana kwenye mchezo wa Serie A Uwanja wa Giuseppe Meazza Jijini
Milan. Mabao mengine ya Inter Milan yalifungwa na Marcelo Brozovic
dakika ya 51, Matias Vecino dakika ya 53 na Stefan de Vrij dakika ya 70
baada ya AC Milan kutangulia kwa mabao ya Ante Rebic dakika ya 40 na
Zlatan Ibrahimovic dakika ya 45 na ushei na kwa ushindi huo sasa kikosi
cha Antonio Conte kinalingana pointi na Juventus, 54 baada ya kila timu
kucheza mechi 23
Home
»
»Unlabelled
» LUKAKU ATIA LA NNE INTER YAITANDIKA MILAN 4-2 SERIE A
Monday, February 10, 2020
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

0 comments:
Post a Comment