MEDDIE
Kagere, mshambuliaji wa Simba amesema kuwa hana habari na tuzo ya
mfungaji bora ila anachotazama ni rekodi mpya kwa timu yake kutwaa taji
la Ligi Kuu Bara.
Simba
imetwaa mataji 20 ya ligi ikiachwa kwa jumla ya mataji 7 na wapinzani
wao Yanga wenye mataji 27, endapo watafanikiwa kulitwaa msimu huu
watabakiza deni la mataji sita kufikia rekodi ya watani zao.
Msimu
wake wa kwanza Bongo 2018/19, Kagere alifunga mabao 23 katika ligi na
timu yake ilitwaa kombe kwa mara ya pili mfululizo ikimaliza na pointi
93, huku ikifunga mabao 77.
Kagere alisema kuwa anashukuru Mungu kwa kumpa nafasi ya kufanya kile anachokipenda akiwa uwanjani jambo ambalo kwake ni furaha.
“Nafasi
yangu na kazi yangu inaniruhusu kufunga na kutengeneza mabao,
ninamshukuru Mungu kwa hili, mashabiki pia nawashukuru kwa kuwa wananipa
sapoti ila nitazidi kupambana kufikia malengo kwani kazi bado
inaendelea,” alisema Kagere

0 comments:
Post a Comment