
Nyota
huyo kutoka kwa Mafarao wa Misri ameshuhudiwa katika msimu wake wa
kwanza ndani ya ‘the Reds’ akipachika kambani jumla ya mabao 44 kwenye
michezo 52 aliyocheza.
Katika msimu
uliyopita Mo Salah, alifunga jumla ya magoli 27 huku hivi sasa
akifumania nyavu mara 18 kiasi kwamba Del Piero amemvulia kofia kijana
huyo.

Akizungumza
na mtandao wa JOE, Del Piero amesema kuwa Salah ni Mungu ‘God’, ”Salah
tayari yeye ni Mungu ‘God’ na hii sio tu kwa Misri.”
”Nakumbuka
wakati alipokuwa Roma, mara kadhaa amekuwa mbele ya goli lakini
alishindwa kufunga. Na ghafla akiwa Liverpool ameonesha uwezo wake kukua
na kufunga zaidi ya magoli 30 kwa msimu.”
Alessandro Del Piero ameongeza ”Unapokuwa kwenye ubora wa namna hii, unahitaji kuimarika, kukuwa na hiko ni kitu kizuri.”
Del
Piero mwenye umri wa miaka 45, amefunga jumla ya magoli 290 kwenye
michezo yake 705 aliyopata kuitumikia klabu ya Juventus na amepata
nafasi ya kumshuhudia Salah wakati huo alipokuwa akicheza ligi ya Serie A
ndani ya klabu ya Roma.
0 comments:
Post a Comment