Aliyekuwa
mchezaji soka maarufu Brazil amezungumza kwa mara ya kwanza tangu
mwanawe wa kiume alipodai kwamba kwasasa huwa hayuko radhi sana kuondoka
nyumbani na kuongeza kuwa hali yake ya afya ni jambo la kawaida kwa mtu
mwenye umri kama wake.
Mtoto wa Pele Edinho
alisema bingwa huyo mara tatu wa kombe la dunia, 79, anaona aibu kutoka
nje ya nyumba yake na pia anahitaji usaidizi wa magongo kutembea
kwasababu ya matatizo yake ya kiafya.
Hatahivyo,
Pele anayetambulika kuwa mchezaji bora amesema: Niko sawa. Ninaendelea
kukubali hali yangu kiafya kwa namna nzuri zaidi na nia yangu ni
kuendelea na maisha yangu kama kawaida."
Pele
alivunja rekodi ya dunia kwa kufunga magoli 1,281 ikiwa ni rekodi ya
duniani katika mechi 1,363 wakati wa kipindi chake cha miaka 21 katika
kandanda, ikiwemo magoli 77 katika mechi 91 akiichezea Brazil.
Mwaka
2015, alifanyiwa upasuaji wa tezi ya kibofu na pia mwaka jana
alipelekwa hospitalini akiwa anaugua maambukizi ya njia ya mkojo.
Marafiki
wa dhati wa Pele aliyekuwa mchezaji wa Santos na New York Cosmos
walisema kwamba Januari mwaka huu ni miongoni mwa miezi ambayo alikuwa
na shughuli nyingi za kufanya.
Upigaji picha na
kazi ya ufadhili anayofanya, Pele anashirikiana na mwelekezi mmoja wa
Uingereza kutengeneza makala kuhusu maisha yake wakati anacheza soka.
"Hata katika ratiba yenye shughuli nyingi bado ninatekeleza majukumu yangu ," amesema hivyo katika taarifa aliyotoa.
"Kuna siku zinakuwa nzuri na nyingine mbaya. Hiyo ni kawaida kwa watu wenye umri kama wangu. siogopi lolote, nimeazimia na ni mwenye matumaini na kile ninachofanya."

0 comments:
Post a Comment