Wednesday, February 19, 2020


MTIBWA Sugar leo imeambulia pointi moja mbele ya Tanzania Prisons kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Mchezo uliopita kwa Mtibwa Sugar ilikubali kichapo cha bao 1-0 mbele ya JKT Tanzania kwa upande wa Tanzania Prisons ililazimisha sare ya bila kufungana na Yanga Uwanja wa Taifa.

Kiungo wa Mtibwa Sugar, Abdulhalim Humud alionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 72 na kuwafanya wamalize wakiwa pungufu ndani ya Uwanja.

Tanzania Prisons ipo nafasi ya 13 ikiwa na pointi 30 huku Mtibwa Sugar ikiwa nafasi ya 15 na pointi 24 na zote zimecheza mechi 23.

0 comments:

Post a Comment