Ole
Gunnar Solskjaer ameshindwa kuvumilia vitimbi vya wakala wa Kiungo
fundi wa United na timu ya taifa ya Ufaransa, Paul Pogba na kusema kuwa
hatma ya nyota huyo ipo mikononi mwa Manchester na sio kwa Mino Raiola.

Wakala
wa Pogba, Mino Raiola mara kadhaa amekuwa akihusishwa na mipango ya
kutaka kumtoa nyota huyo ndani ya Old Trafford, na kumpeleka katika
klabu nyingine.

Wakala wa Pogba, Mino Raiola
Mfaransa
huyo amekuwa akisumbuliwa na majeraha mara kadhaa msimu huu, United na
Raiola tayari wamegombana mwaka huu baada ya klabu hiyo ya Premier
League kushindwa kumsajili Erling Haaland.
”Paul
ni mchezaji wetu na sio wa Mino Raiola, sijakaa na Pogba kumuambia
anachosema wakala wake,” amesema Solskjaer katika mkutano na waandishi
wa habari.

Paul Pogba mara ya mwisho kushuka dimbani ilikuwa siku ya ‘Boxing Day’ akitumia dakika 45 kwenye mchezo ambao walishinda jumla ya magoli 4-1 dhidi ya Newcastle
0 comments:
Post a Comment