Tuesday, February 18, 2020


Tottenham na Everton wanamuwania beki wa Manchester United Chris  Smalling, 30, ambaye anachezea kwa mkopo na klabu Roma. (Corriere dello Sport – in Italian)
Chris Smalling
Kiungo Mfaransa Matteo Guendouzi, 20, anakabiliwa na mapambano ya kusalia katika klabu ya Arsenal baaada ya kuachwa kwenye kikosi cha klabu hiyo kwenye mchezo wa Jumapili dhidi ya Newcastle. (Mirror)
Guendouzi aliachwa baada ya kugombana na kocha wa Arsenal Mikel Arteta na makocha wasaidizi wakati wa mapumziko mafupi ya katikati ya msimu jijini Dubai. (Goal)SterlingKiu ya Sterling kunyakua Champions League itabaki kuwa ndoto kwa miaka mitatu ijayo.
Winga Raheem Sterling, 25, ataendelea kusalia Manchester City licha ya klabu hiyo kupigwa marufuku kushiriki michuano ya Ulaya, amedai wakala wake. (Manchester Evening News)
Barcelona wanatarajiwa kufanya usajili wa dharura kwa kumnyakua mshambuliaji wa zamani wa Middlesbrough Martin Braithwaite, 28, kutoka klabu ya Leganes. (Mundo Deportivo, via Teeside Gazette)WernerWerner (kushoto) yupo kwenye rada za Klopp licha ya mazungumzo rasmi ya usajili kutoanza.
Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp yungali anavutiwa na mshambuliaji wa Kijerumani Timo Werner, 23, lakini bado klabu hiyo haijaanzisha mazungumzo na RB Leipzig juu ya usajili wa nyota huyo. (Independent)
Kocha wa klabu ya Lille ya Ufaransa, Christophe Galtier anadai hakuna uhasama baina ya klabu hiyo na kiungo wake Mfaransa Boubakary Soumare, 20, ambaye anawania na vilabu vya Manchester United, Liverpool na Chelsea. (Express)

0 comments:

Post a Comment