KOCHA
Mkuu wa Yanga, Mbelgiji Luc Eymael amesema kuwa ana imani kikosi chake
kitamaliza msimu huu wa Ligi Kuu Bara katika nafasi ya pili
inayoshikiliwa na Azam FC yenye pointi 54.
Eymael
amesema kuwa itakuwa ni kujiongopea kwa sasa akisema kuwa anahitaji
kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara kutokana na kuachwa na wapinzani wake
Simba ambao wapo nafasi ya kwanza.
Simba
inaongoza ligi ikiwa na pointi 71 baada ya kucheza mechi 28 huku Yanga
ikiwa nafasi ya tatu na ina pointi 51 baada ya kucheza mechi 27.
Namungo FC ipo nafasi ya nne ikiwa imejiwekea kibindoni pointi 50.
Eymael
amesema: "Ninatambua kwamba mashabiki wanahitaji kuona timu inatwaa
ubingwa lakini kwa sasa malengo yangu makubwa ni kuona timu inamaliza
ikiwa nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi.
"Hilo
lipo mkononi mwetu ukizingatia kwamba wachezaji wamekuwa na morali
nzuri na maendelea yanaonekana nina amini kwamba kila mmoja atafurahi
kuona namna ambavyo tutafikia malengo tuliyojiwekea," amesema.
Yanga
imebakiza mechi 11 mkononi ili kumaliza ligi ambayo imesimama kwa muda
kwa ajili ya kuzuia maambukizi ya Virusi vya Corona.
0 comments:
Post a Comment