MARA
baada ya tarehe ya kurejea kwa Ligi Kuu ya England ‘Premier League’
kusogezwa mbele kutoka Aprili 4 hadi Aprili 30, kutokana na hofu ya
Ugonjwa wa COVID-19 unaotokana na Virusi vya Corona, imebainika kuwa
kuna gharama kubwa nyuma yake.
Ligi
hiyo ambayo ina mikataba mingi inaweza kuwapa hasara uongozi wa Premier
League kama itatokea ligi hiyo itashindwa kurejea kama kawaida.
Imeelezwa
kuwa gharama ya kutomalizika kwa ligi hiyo kutasababisha uongozi wa
Premier ulipe pauni 762m (zaidi ya Sh trilioni 2) kama malipo ya
kuvunjwa kwa mkataba wa kutomalizika kwa msimu wa 2019-20.
Ligi
hiyo na nyingine zote zimesimamishwa kupisha maambukizi ya Virusi vya
Corona ambavyo vimekuwa vikisambaa kwa kasi nchini England huku kukiwa
hakuna tiba iliyopatikana.
Vituo
ambavyo vimelipia malipo ya msimu mzima ikiwemo Sky Sports vinahaha
kuhakikisha mikataba ya matangazo inawekwa sawa kwa kuwa malipo
yameshafanyika na mambo hayajaenda sawa. Malipo ya haki za matangazo
huwa yanafanyika mapema na baadhi huwa yanatolewa kwa klabu mwanzoni mwa
msimu.
Njia
pekee ambayo inaweza kupunguza makali ya kulipa fidia hiyo ni michezo
kuendelea kwa kuchezwa bila mashabiki ili angalau yale makampuni
yaliyolipia haki za matangazo yasiishitaki Premier League. Klabu
zinahitaji malipo ya haki za kuonyeshwa kwa michezo yao ili ziwasaidie
katika malipo ya mishahara ya wachezaji wao wakati huu ambapo ligi
zimesimama
0 comments:
Post a Comment