
Baba wa mchezaji wa
Real Madrid Luka Jovic, 22, amesema mtoto wake inabidi akubali adhabu
yoyote - hata kufungwa- endapo atakutwa na hatia ya kukiuka masharti ya
karantini kwa kusafiri kwenda kumtembelea mpenzi wake jijini Belgrade.
(Marca)
Barcelona wana nia ya kumsajili beki wa Manchester City na
Ufaransa Aymeric Laporte, 25, katika majira ya kiangazi.(Mundo
Deportivo - in Spanish)Klabu za Paris St-Germain, Real Madrid na Manchester City zote zinawania kumsajili beki wa Inter Milan na timu ya taifa ya Slovakia Milan Skriniar, 25. (Calciomercato - in Italian)

- Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 22.03.2020
- Michuano ya Olimpiki mbioni kuahirishwa kwa hofu ya Coronavirus

Arsenal wapo katika mazungumzo na madaktari wa klabu nyengine za Ligi ya Premia juu ya uwezekano wa wachezaji wake kuanza mazoezi wiki hii. (Mail)

Barcelona wapo katika mazungumzo na wachezaji wao nyota ili kupunguza mishahara yao kutokana na klabu hiyo kuona kuwa haitaweza kuhimili bajeti ya mishahara inayofikia Euro bilioni 1 kwa kipindi cha msimu kilichobakia. (Marca)
Kiungo wa zamani wa Arsenal na Barcelona Alexander Hleb amedai "hakuna mtu anayejali" kuhusu virusi vya corona nchini mwake Belarus nchi pekee ambayo bado inaendelea na ligi kuu kwa sasa. (Sun)
0 comments:
Post a Comment