Nyota wa zamani wa soka wa Brazil, Ronaldinho na kaka yake wamekamatwa wakituhumiwa kutumia hati bandia za kusafiria kuingia nchini Paraguay, mamlaka zimesema.
"Ronaldinho atahojiwa saa 2:00 asubuhi leo Alhamisi katika ofisi ya mwendesha mashtaka," Waziri wa Mambo ya Ndani, Euclides Acevedo aliwaambia waandishi wa habari.
Polisi wa Paraguay walivamia hoteli jijini Asuncion ambako mshindi huyo wa tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia ya mwaka 2005 alikuwa akiishi akiwa safari yake ya kutangaza kitabu, na wakakuta nyaraka hizo za kughushi, waziri huyo alisema.
"Pia tunachunguza uwajibikaji wa mamlaka zilizomruhusu kuingia nchini kwa kutumia hati feki za kusafiria," alisema Acevedo.
0 comments:
Post a Comment