
Image caption Winga wa Borussia Dortmund Jadon Sancho hana hofu kuhusiana na hatma yake ya baadae katika klabu hiyo
Winga wa Borussia
Dortmund Jadon Sancho, 19, hana mawazo kuhusiana na hatma yake ya baadae
licha ya tetesi zinazomhusisha na uhamisho wa kuenda Manchester United
ama Liverpool. (Mail)
Tottenham wanajiandaa kumsaka kipa wa
Watford Ben Foster, 36, ambaye mkataba wake Vicarage Road unamalizika
msimu huu wa joto. (Sun)Spurs pia wanataka kuikosesha Roma nafasi ya kumpata Chris Smalling kutoka Manchester United kwani wana mpango wa kumpatia mkataba wa kudumu.
Beki huyo wa England, 30 ,kwa sasa yuko katika klabu hiyo ya Italia kwa mkopo. (Calciomercato, in Italian)

United pia wanamfuatilia beki wa Stoke City Nathan Collins, Kiungo huyo wa kimataifa wa Jamhuri ya Ireland aliye na umri wa chini ya miaka 21, amecheza mara 12 katika timu ya kwanza ya Potters. (Sun)
Dries Mertens ,31, anayelengwa na Chelsea anakaribia kusaini mkataba mpya katika klabu ya Napoli. Mkataba wa mshambuliaji huyo wa Ubelgiji inakamilika msimu huu wa joto. (Sun)

Afisa mkuu mtendaji wa Inter Milan Giuseppe Marotta anahofia msimu wa ligi kuu ya Italia Serie A huenda usimaliziki ikiwa hawatapata suluhisho janga la kiafya la coronavirus. (Mail).
Tetesi Bora Jumapili
Cristiano Ronaldo, 35, amesema kwamba anafurahia kuwa Juventus na hana nia ya kujiunga na Inter Miami inayomilikiwa na David Beckham. (Sky Sports)Barcelona inamnyemelea mshambuliaji wa Arsenal Pierre-Emerick Aubameyang, 30 ambaye mkataba wake unamlizika mwisho wa simu ujao. (Sunday Express)

Mshamambuliaji wa Borussia Dortmund, Erling Braut Haaland ndiye anayependelewa na Real Madrid wakati inapojiandaa kuongeza mshambuliaji mwengine kwa msimu wa tatu mfululizo.
Mshambuliaji wa RB Leipzig Timo Werner, 23, pia yuko kwenye orodha ya Real Madrid na kumaanisha kwamba huenda Liverpool ikapata upinzani wa kumpata mchezaji huyo wa Ujerumani. (Daily Mail)

Liverpool itakuwa na kibarua cha kuimarisha safu yake ya mashambulizi msimu ujao kwasababu mchezaji wa kimataifa Adam Lallana, 31, na Xherdan Shaqiri, 28, wa Switzerland wote wanatarajiwa kuondoka mwisho mwa msimu. (The Athletic via Express)
0 comments:
Post a Comment