
Mshambuliaji wa
Manchester United na Nigeria Odion Ighalo, 30, ambaye yuko klabu hiyo
kwa mkopo kutoka Shanghai Shenhua, anajiandaa kupunguziwa mshahara hadi
£6m ili asalie katika ligi ya primia. (Mail)
Klabu hiyo
inayochezea Old Trafford pia inapigiwa upatu kusajili kiungo wa kati wa
Ajax Donny van de Beek, nayo Real Madrid huenda ikamkosa kiungo wa
kimataifa wa Uholanzi wa miaka 23. (Marca - in Spanish)Juventus inajiandaa kuwasilisha ofa ya kumnunua mshambuliaji wa Portugal Cristiano Ronaldo, 35, mkataba ambao utarefusha uwepo wake katika klabu hiyo ya Italia hadi mwaka 2024. (Tuttosport via Mail)

Manchester City wanatumia muda uliowekwa wa kuahirisha ligi ya Primia kujadili mkataba mpya wa wachezaji Kevin De Bruyne, 28, na Raheem Sterling, 25. (Sun)
Mkufunzi wa Arsenal Mikel Arteta anamtaka beki wa West Ham ambaye thamani yake inakadiriwa kuwa £60m Issa Diop, 23, ambaye pia ananyatiwa na Manchester United. (Metro)

Barcelona, Manchester United na Real Madrid zitamenyana kumpata kiungo wa kati wa Fenerbahce Mturuki Omer Beyaz, 16. (Express)
Kipa wa mkopo wa Sheffield United Dean Henderson, 23, anatarajiwa kurejea katika klabu yake ya Manchester United msimu wa joto licha ya Chelsea kuonesha nia ya kutaka kumnunua. (Star)

Mashabiki wametoa wito kwa wamiliki wa West Ham, David Sullivan na David Gold kuuza klabu hiyo licha ya ongezeko la kutoridhishwa kwao na utendakazi wake. (Telegraph)
Klabu kadhaa za Ulaya zilizo na wachezaji wa hadhi ya juu waliojeruhiwa huenda zikafaidi mapumziko yaliyotokana mlipuko wa coronavirus. (Mail)
0 comments:
Post a Comment