KIRAKA wa Simba, mkongwe Erasto Nyoni amesema kuwa bado kidogo wachezaji wataendelea kurejea kwenye ubora wao kutokana na kuanza kufanya mazoezi ya pamoja.
Nyoni jana Mei 27 alikuwa miongoni mwa wachezaji walioripoti kambini na kuanza mazoezi pamoja na wachezaji wenzake kujiandaa na mechi za kumalizia ligi pamoja na Kombe la Shirikisho.
Masuala ya michezo yalisimamishwa Machi 17 na Serikali kutokana na maabukizi ya Virusi vya Corona kutikisa dunia na Serikali imeruhusu kuanza kwa michezo ifikapo Juni Mosi.
Tayari Bodi ya Ligi Tanzania imetoa taarifa kuwa mechi za ligi zitaanza kuchezwa Juni 13 huku ratiba ikitarajiwa kutangazwa Jumapili.
0 comments:
Post a Comment