Everton
imewasilisha ombi la £40m kumsaini kiungo wa kati wa Napoli, Allan, 29,
lakini klabu hiyo inataka dau la £60m kumuuza raia huyo wa Brazil. (Il
Mattino - in Italian)
The Toffees pia wamewasilisha ombi la $25m
kwa Barcelona kumnunua beki wa Ufaransa Jean -Claire Todibo ,20, ambaye
kwa sasa anahudumu kwa mkopo katika klabu ya Schalke nchini Ujerumani.
(Mail)Manchester United itamuongezea kandarasi kipa wa England Dean Henderson, 23 ili kumruhusi kumaliza msimu wake na klabu ya Sheffield United huku kandarasi yake ikitarajiwa kukamilika mwezi Juni. (Telegraph)
Mmiliki wa Bournemouth Maxim Demin karibu aiuze klabu hiyo kwa mfanyabiashara wa Saudia mnamo mwezi Januari , kabla ya makubaliano hayo kugonga mwamba kuhusiana na thamani ya klabu hiyo. (90min)
Kiungo wa kati wa Brazil Phillipe Coutinho ambaye yuko kwa mkopo katika klabu ya Bayern Munich huenda asicheze tena baada ya klabu hiyo ya Bundesliga kuamua kutomsaini kwa mktaba wa kudumu kutoka Barcelona, na sasa ananyatiwa na Chelsea, Arsenal na Tottenham. (Sky Sports)
Chelsea imeamua kutotumia kifungu chake cha sheria dhidi ya winga wa Ivory Coast Jeremie Boga ,20, ambaye amehusishwa na uhamisho wa kwenda kuichezea klabu ya Napoli. (Guardian)
Mshambuliaji wa Inter Milan na Argentina Mauro Icardi, 27, anakaribia kuhamia katika klabu ya Paris St-Germain kwa dau la £54m. (ESPN)
Paris St-Germain inafanya mazungumzo na Arsenal katika jaribio la kumsaini mashambuliaji wa klabu hiyo Pierre-Emerick Aubameyang, 30, kwa£34m. (Todofichajes)
Tetesi za Soka Jumatatu
Mshambuliaji wa Juventus Gonzalo Higuain, 32, huenda akarudi katika ligi ya premia baada ya uhamisho wake wa mkopo katika klabu ya Chelsea - Newcastle na Wolves zote zinamwania. (Express)Juventus inataka kuipiku Real Madrid katika ununuzi wa mshambuliaji wa Borussia Dortmund Erling Braut Haaland, 19, katika uhamisho wa dau la £67m. (Tuttosport - in Italian)
Barcelona iko tayari kumuuza mashambuliaji wa Ufaransa Ousmane Dembele, 23, kwa dau la £37m. Klabu hiyo ya Uhispania ililipa £137m kumnunua raia huyo wa Ufaransa miaka mitatu iliopita lakini ameanzishwa mara tano pekee kufuatia msururu wa majeraha. (Mirror)
Mshambuliaji wa klabu ya RB Leipzig Timo Werner, 24, amehusishwa pakubwa na uhamisho wa kujiunga na Liverpool lakini aliyekuwa mchezaji wa zamani wa Manchester United Owen Hargreaves anahisi kwamba uhamisho wa klabu hiyo ya Old Trafford ungekuwa bora zaidi kwa mchezaji huyo. (Star)
0 comments:
Post a Comment