Tuesday, May 26, 2020


Mechi ya mahasimu Real Betis na Sevilla inatarajiwa kufungua dimba la kurejea kwa msimu wa Ligi Kuu ya Kandanda ya Uhispania mnamo Juni 11.
La Liga yapangwa kurejea Juni 11
Kama ilivyo kwa ligi nyengine ulimwenguni, ligi hiyo maarufu kama La Liga ililazimika kusimamishwa mwezi Machi kwa muda usiojulikana kutokana na mlipuko wa virusi vya corona. Ligi hiyo pia itarejea kwa michezo ambayo haitahudhuriwa na mashabiki uwanjani kama ilivyo kwa Ujermuani.
Mkuu wa La Liga Javier Tebas ameiambia runinga moja nchini Uhispania kuwa mechi hiyo "itakuwa ni tuzo maalumu kwa wote waliofariki".
Hata hivyo, Tebas amewaonya wachezaji wawe "waangalifu na matendo yao" baada ya wachezaji wanne wa Sevilla kuomba radhi kwa kuvunja masharti ya kujiteng katika jamii.
Wachezaji hao Ever Banega, Lucas Ocampos, Franco Vazquez na Luuk de Jong walipigwa picha katika mjumuiko wa sherehe mwishoni mwa wiki.
Uhispania umelegeza masharti ya marufuku ya watu kutokutoka nje, lakini mikusanyiko ya Zaidi ya ya watu 10 badoo ni marufuku.
"Wachezaji ni mfano kwa jamii, na wanapaswa kuwa makini na matendo yao," ameeleza Tebas.
"Nawataka wachezaji wote kutokuwa kama hivi. Inatubidi tuwe makini kwa kuwa ajira za watu wengi zipo hatarini."
Siku ya Jumamosi, Waziri Mkuu wa Uhispania Pedro Sanchez alitoa ruhusa kwa ligi za juu za kandanda kurejea nchini humo kuanzia Juni 8.
Wachezaji wa La Liga walianza mazoezi katika makundi ya wachezaji wasiozidi 10 wiki iliyopita. Tabias anaeleza kuwa lengo sasa ni kurejesha mazoezi kamili.
"Kwa sasa hilo ndilo lengo letu, na tukishafanikisha hilo tutaweza kuirejesha ligi. Shabaha yetu ni kutangaza tratiba ya mizunguko ya mechi wiki ijayo."
"Tangazo la serikali lilitushtua, laikni linaonesha ni kwa namna gani mpira wa kulipwa ni muhimu sana kwa nchi hii."
Miamba Barcelona inaongoza ligi hiyo kwa alama mbili mbele ya Real Madrid huku kukiwa na mechi 11 ili kukamilisha msimu.
Wachezaji wa ligi mbili madaraja ya juu waliweza kurejea katika mazoezi binafsi mapema mwezi huu wa Mei baada ya kufanyiwa vipimo vya corona.
Wachezaji watano walikutwa na virusi katika ligi hizo mbili na wakajitenga karantini kabla ya ruhusa ya mazoezi ya makundi kuanza Mei 18.
Wakati huo huo, Ligi Kuu ya Ureno inatarajiwa kurejea Juni kwa michezo miwili. Klabu ya Portimonense itaminyana na Gil Vicente huku Famalicao ikiwakaribisha vinara Porto.
Porto wapo kileleni kwa tofauti ya alama moja dhidi ya mahasimu wao Benfica huku mechi 10 zikisalia kabla msimu ufikie tamati.
  • 0 comments:

    Post a Comment