Uongozi
wa Azam FC imesikitishwa sana na tabia ya Klabu ya Yanga ambayo
wamefanya leo ya kumuandikia Barua mchezaji wa Klabu hiyo Salum Abubakar
Sure boy ya kuomba kuondoka ndani ya Klabu hiyo .
Zaka Zakazi amesema kuwa Barua hiyo iliyowasilishwa leo ina makosa mengi kwani imewasilishwa na Mtu wa Yanga ambaye alikuwa anapeleka Barua za ofa za kumtaka Sure boy mwanzoni na imeandikwa tarehe 12/08/2020 ikiwa leo ni tarehe 11/08/2020.
Klabu ya Yanga imetengeneza Barua ya Salum Abubakar na pia wamefanya mazungumzo na mchezaji ambaye ana mkataba. Zaka amedai Klabu ya Yanga haipaswi kuongea na mchezaji ambaye ana mkataba hivyo Yanga wamefanya makosa.
Afisa Habari wa Klabu hiyo Zaka Zakazi imeitaka klabu ya Yanga itoke hadharani na kuiomba radhi klabu ya Azam haraka iwezekanavyo kwa ilichokifanya kwani mchezaji wao (Sure boy) ameikana barua hiyo.
0 comments:
Post a Comment