Kiungo
wa Yanga, Morrison alikuwa na mvutano mkubwa na klabu ya yake kuhusu
sakata la mkataba ambapo yeye anadai kwamba ana dili la miezi sita
ambalo limekwisha huku Yanga ikieleza kuwa ana dili la miaka miwili.
Sakata
lake leo ni siku ya pili ambapo lilianza kusikilizwa jana, Agosti 10 na
leo Agosti 11 pia limeskilizwa na hakuna majibu ambayo yametolewa.
Mwanjala
amesema kuwa kuna document moja haijakamilika kwa pande zote mbili ya
Yanga na Morrison na pande zote zimesema jioni ya leo watazileta.
"Kuna
nyaraka ambazo hazijakamilika kwa pande zote mbili, moja ya Yanga na
moja ya Morrison jambo ambalo limefanya tushindwe kutoa maamuzi.
"Kesho
zitakabidhiwa kwa kamati ambapo kikao kitaanza kesho saa 4 asubuhi
kufikia saa saba na nusu kesho kikao kitakuwa kimekwisha na watatoa
maamuzi juu ya kesi hiyo."
Morrison
Agosti 8 kesi yake ikiwa bado haijatolewa hukumu alitambulishwa na
watani wa jadi Simba huku ikielezwa kuwa amesaini kandarasi ya miaka
miwili jambo linaloongeza mvutano wa uhalali wake.
0 comments:
Post a Comment