HASSAN
Mwakinyo, bondia wa ngumi za kulipwa Mtanzania anayeipeperusha vema
Bendera ya Taifa kwenye ndondi, usiku wa kuamkia leo amemnyoosha kwa
pointi Tshibangu Kayembe raia wa Congo.
Mwakinyo ameshinda kwa pointi pambano hilo la raundi 12 la uzito wa Super Welter katika kuwania mkanda wa Ubingwa wa Dunia wa WBF.
Mabondia
hao walionekana kukamiana na kushushiana vitasa vikalivikali katika
pambano hilo lililofanyika Ukumbi wa Mlimani City Dar na kuhudhuriwa na
wadau wengi.


Baada
ya ushindi huo mgeni rasmi Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na
Michezo, Juliana Shonza alimvalisha Mwakinyo mkanda huo na kumtawaza
Ubingwa mpya wa mkanda huo wa WBF.
Waziri Shonza amesema anampongeza Mwakinyo kwa kuutetea mkanda huo uliopambaniwa nyumbani na kuiletea nchi sifa.
Mhariri
Mtendaji wa Kampuni ya Global Group, Saleh Ally, wachapishaji wa
magazeti ya michezo ya Spoti Xtra na Championi ambao walikuwa ni
wadhamini wa pambano hilo amesema kuwa Mwakinyo anastahili pongezi kwa
kupambana na kupata ushindi.
0 comments:
Post a Comment