Wednesday, August 5, 2020



IMEELEZWA kuwa Sh 60Mil za kuuvunja mkataba kwenye klabu yake ya KMC, ndizo zimechelewesha mipango ya Yanga kufanikisha usajili wa beki wa kulia wa timu hiyo, Kelvin Kijiri.

 Kijiri amekuwa akipata nafasi ya kukitumika kikosi ccha timu ya Taifa ya Tanzania na Klabu yake ya KMC, ni kati ya wachezaji wanaotajwa kujiunga na Yanga.

Nyota huyo anayecheza beki wa kulia, anatarajiwa kujiunga na Yanga kwa ajili ya kusaidiana na nahodha mkongwe Juma Abdul baada ya Paul Godfrey ‘Boxer’ kuonekana kupoteza nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza.

KMC ndiyo imeipa ugumu Yanga kushindwa kukamilisha dili hilo la usajili baada ya klabu kutaka Sh milioni 60 za kuvunja mkataba nje ya mchezaji mwenyewe.

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa kutokana na klabu kuhitaji fedha hizo za kuvunja mkataba wa mwaka mmoja, matajiri wa Yanga ambao ni GSM waliobeba jukumu la kusimamia usajili, wamefikia makubaliano ya kuachana na beki huyo.

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa uongozi wa Yanga upo tayari kutoa dau hilo la fedha kwenda kwa mchezaji pekee na siyo kumalizana na klabu hiyo inayommiliki.

Aliongeza kuwa uongozi upo kwenye mazungumzo na baadhi ya mabeki wengine wa kulia kutoka ndani ya nchi.

“Uongozi wa Yanga umesitisha mipango ya kumsajili Kijiri tuliyekuwa kwenye mipango naye ya kumsajili katika kuelekea msimu ujao, hivyo hivi sasa tupo kwenye mazungumzo na baadhi ya wachezaji wengine wenye uwezo na ubora wa kuichezea Yanga.

“GSM wapo tayari kutoa kiasi hicho cha fedha kwa kumpatia mchezaji pekee na siyo kuipa klabu, hivyo mchezaji mwenyewe anatakiwa kuzungumza na waajiri wake kabla ya kuja kwetu.

“Wapo wachezaji wengi wenye uwezo wa kucheza nafasi hiyo, hivyo tunaamini tutampata,” alisema mtoa taarifa huyo.

Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM, Injinia Hersi Said alisema: “Asilimia mia moja tumefikia pazuri na baadhi ya wachezaji tuliokuwa nao kwenye mazungumzo ya awali, hivi sasa tunamalizana na waajiri wao kwa wale wenye mikataba kwa ajili ya kuivunja, nisingependa kuwaweka wazi ni akina nani kwa hivi sasa.”

0 comments:

Post a Comment