Mshambulaji
Romelu Lukaku akishangilia baada ya kuifungia Inter Milan bao la pili
dakika ya 21 katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Bayer Leverkusen kwenye
mchezo wa mkondo mmoja wa Robo Fainali ya UEFA Europa League usiku wa
jana Uwanja wa Merkur Spiel-Arena Jijini Dusseldorf, Ujerumani. Bao la
kwanza la Inter Milan lilifungwa na Nicolo Barella dakika ya 15, wakati
la Bayer Leverkusen lilifungwa na Kai Havertz dakika ya 24 na sasa
kikosi cha Antonio Conte kitakutana na mshindi kati ya Shakhtar Donetsk
na Basel zinazomenyana leo katika Nusu Fainali Jumapili

0 comments:
Post a Comment