Tuesday, August 18, 2020


 


SAID Ndemla, kiungo mkabaji ndani ya Klabu ya Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck, leo Agosti 18 ameongeza kandarasi ya miaka miwili kuendelea kutumika ndani ya klabu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Msimbazi.

Msimu wa 2019/20, Ndemla amekuwa hana nafasi kikosi cha kwanza akijenga urafiki mkubwa na benchi huku nafasi yake ya ukabaji ikiwa mikononi mwa Jonas Mkude.

Kwenye mabao 78 ambayo yamefungwa na Simba amehusika kwenye mabao mawili ambapo alifunga bao moja na kutoa pasi moja ya bao.

Simba ikiwa imecheza jumla ya mechi 38 amecheza mechi 10 za Ligi Kuu Tanzania Bara.

 

0 comments:

Post a Comment