Klabu ya Yanga wanatarajia kuweka bayana majina ya wachezaji watakaobaki
katika kikosi hicho na wale watakaoachwa huku pia wakitangaza maingizo
mapya ndani ya kikosi hicho.
Mwenyekiti wa kamati ya usajili wa klabu hiyo Hussein Nyika ameeleza
hayo huku akisisitiza kuwa staili yao ya kusajili ni ile ile ya kimya
kimya na hawataki kuonesha tambo zozote.
"Tunasajili kimya kimya na mambo yetu yote yatakuwa hadharani pindi
kocha wetu atakaporejea kutoka Ufaransa, kila kitu kinaenda sawa na watu
wawe watulivu", amesema Nyika.
Nyika ameongeza "Kuhusu wachezaji wetu waliomaliza mikataba tupo katika
harakati za kuwaongeza kama kocha bado atakuwa na matumizi nao na
akarudi tutatangaza wanaobaki na watakaopelekwa klabu zingine kwa
mkopo".
Yanga wanajiandaa na mchezo wa hatua ya makundi katika kombe la
Shirikisho barani Afrika huku wakitarajia kukipiga na Gor Mahia ya
nchini Kenya Julai 18 mwaka huu.
Home
»
»Unlabelled
» Yanga Kukitangaza Kikosi Watakachobaki Nacho Wiki Hii
Wednesday, June 20, 2018
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment