NI kama uongozi wa Kagera Sugar umeamua kumruhusu mlinda mlango wao
mahiri, Juma Kaseja, kujiunga na timu yoyote ambako ataona yeye kunamfaa
baada ya kushindwana na uongozi wa timu hiyo.
Kaseja ambaye alishawahi kuzitumikia klabu za Simba na Yanga kabla ya
kujiunga na Mbeya City na kisha kujiunga na Kagera Sugar ameshaelezwa
kuwa anaweza kuondoka hapo.
Akizungumza na Championi Jumatano, Meneja wa Kagera Sugar, Mohamed
Hussein, alisema kuwa walikaa kikao jana kujadili juu ya kuongeza
wachezaji wapya katika timu yao baada ya kocha wao kuwasilisha ripoti
yake juzi.
“Mwalimu alitupatia ripoti Jumapili baada ya kumaliza sikukuu ya Eid na
Jumatatu tulikaa kikao na viongozi wengine na yeye kocha (Mecky Mexime),
nadhani hatutasajili wachezaji wengi ila tutaangalia wachezaji ambao
wataondoka, lazima tuangalie wachezaji mbadala.
“Juma Kaseja tupo naye kwenye mazungumzo, lakini kama atapata timu ya kwenda, tunamruhusu kwenda.
“Sisi tunaamini kuna wachezaji wengi wenye kipaji kama Kaseja, hatuwezi kumlazimisha mchezaji kama anataka kuondoka.
“Sisi siyo kama timu nyingine kwamba tunapatana na mchezaji tutampa
kiasi hiki, hatuwezi kuvuka hapo hata aje nani na huo ndiyo utaratibu
wetu, sasa kama ameona sehemu kuna maslahi sisi tunamruhusu kwenda,”
alisema.
Install Application ya Udaku Special Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi
Home
»
»Unlabelled
» Kagera Sugar Yashindwana na Kaseja Yamruhusu Kwenda Popote
Wednesday, June 20, 2018
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment