Tuesday, September 15, 2020


 

Timu ya Manispaa ya Kinondoni, KMC FC imeanza kufanya mazoezi yake ya kawaida ikiwa ni katika maandalizi ya mchezo wake dhidi ya Mwadui FC ya Mkoani Shinyanga Septemba 21 mwaka huu.

KMC FC itakutana na Mwadui katika uwanja wa Mwadui Complex ambapo itakuwa ugenini dhidi ya mchezo huo huku ikihitaji ushindi kwa lengo la kuendelea kujiweka katika nafasi ya kuongoza ligi kuu Tanzania bara msimu wa mwaka 2020/2021.

Kupitia mazoezi hayo kikosi hicho kitaendelea kujiimarisha  zaidi  kwakucheza mechi za kirafiki kabla ya kukutana na Mwadui FC jambo ambalo litaiwezesha kujiweka tayari katika mchezo huo.

Aidha KMC hivi sasa inaongoza ligi ikiwa imejikusanyia point sita na magoli sita  katika michezo yake miwili ambapo Septemba saba  ilikutana na Mbeya City katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam na kuibuka na ushindi wa goli nne kwa nunge, Septemba 12 ilicheza na Tanzania Prisons na kuibuka na ushindi wa goli mbili kwa moja

 

0 comments:

Post a Comment