YANGA SC kupitia kwa Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM, Eng. Hersi Said, wamethibitisha kuwa beki wao wa kimataifa, Mghana Lamine Moro ameongeza mkataba wa kuichezea Yanga hadi 2023.
Lamine Moro ameongeza mkataba wa kuwatumikia mabosi wake Yanga hadi mwaka 2023.
Lamine,
raia wa Ghana hivi karibuni iriripotiwa kuwa mkataba wake unakaribia
kufika ukingoni jambo ambalo limewafanya mabosi wake kumpa dili jipya
kutokana na uwezo wake kuwa ndani ya uwanja.
Lamine amesema:-"Ni kweli nimeona vyema kuongeza mkataba, kwanza itanipa muda zaidi wa kutekeleza majukumu yangu.
"Ninapenda
kuwaambia mashabiki kuwa ni muhimu kuendelea kushikamana.Nina furaha
kubwa ya kuongeza mkataba ndani ya Yanga pamoja.Kuaminiwa na mashabiki
pamoja na uongozi kwangu ni furaha nitazidi kupambana kufanikisha
malengo ya timu."
Beki
huyo kisiki alijiunga Yanga kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Bidcom
ya Zambia mkataba wake wa awali unamalizika mwishoni mwa msimu uja
mwaka 2021. Hivyokwa kusaini kwake dili jipya kunamfanya Lamine
kuendelea kubaki mitaa ya Jangwani hadi Julai 2023.
Ndani
ya Ligi Kuu Bara akiwa amecheza mechi tatu msimu wa 2020/21 amefunga
mabao mawili akiwa ni kinara wa kutupia mabao ndani ya Yanga iliyofunga
mabao manne ikiwa imecheza mechi nne.

0 comments:
Post a Comment