
Chanzo cha picha, Reuters
Lionel Messi has spent his entire career with Barcelona
Lionel Messi aliichezea kwa mara ya kwanza Barcelona tangu jaribio lake la kutaka kuondoka kugonga mwamba akishiriki katika mechi ya kirafiki dhidi ya klabu ya Gimnastic de Tarragona.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 aliwasilisha ombi la kutaka kuondoka katika klabu hiyo mwezi Agosti lakini akaamua kusalia kwasababu hakuna klabu ingeweza kutoa fedha za kifungu cha sheria cha kumuondoa katika klabu hiyo.
Messi alianza katika mechi hiyo ambapo Barcelona ilijipatia ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya klabu ya ligi ya daraja la tatu Nastic baada ya klabu hiyo kuthibitisha kwamba atasalia kama nahodha wake.
Alipumzishwa pamoja na wachezaji walioanzishwa katika kipindi cha kwanza.
Ousmane Dembele alifunga goli la kwanza huku Antoine Griezman na Phillipe Coutinho wakifunga magoli ya penalti.
Messi ambaye ni mfungaji wa magoli mengi katika klabu ya Barcelona aliamini kwamba alikuwa na kifungu cha sheria katika kandarasi yake ambacho kingemruhusu kuondoka kama ajenti huru hivyobasi hakujiandaa kwa mazoezi ya kufungua msimu.
Barcelona na ligi ya La Liga zilisisitiza kwamba sheria hiyo ni sharti ifuatwe na kwamba klabu yoyote ambayo inataka kumnunua nyota huyo italazimika kulipa £624m - Na Messi akalazimika kurudi katika mazoezi baada ya kusema kwamba hataishtaki klabu hiyo.
Msimu wa Barca unaanza siku ya Jumapili tarehe 27 mwezi Septemba na mechi ya nyumbani dhidi ya Villareal.
0 comments:
Post a Comment