MANCHESTER United inasemekana wana imani watamsajili Jadon Sancho kabla ya dirisha la usajili kufungwa.
Meneja
wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer amemwambia nyota wa Borussia
Dortmund, Jadon Sancho kuwa dili lake la kujiunga na United
litakamilika kwa mujibu wa ripoti ya Dagbladet.
Mpaka
sasa United walishindwa kutoa fedha ya pauni milioni 108 ambayo
Dortumund wanahitaji ili wamuachie kiungo Sancho mwenye uwezo mkubwa
ndani ya uwanja.
Dirisha la usajili litafungwa Oktoba 5 lakini, Solskjaer anaonekana kuwa na ujasiri wa wa kumpata Sancho ambae ndio tageti yake ya kwanza msimu huu.
Miongoni
mwa dili ambalo limezungumzwa kwa muda wote na halijaonesha mafanikio
ndani ya united ni la nyota huyu aliyefunga jumla ya mabao 20 msimu
uliopita na kutoa pasi 20 kwenye mashindano yote.

0 comments:
Post a Comment