Friday, September 18, 2020


Watford inataka pauni milioni 36 kwa ajili ya mshambuliaji Ismaila Sarr

Liverpool wamemfuatilia Ismaila Sarr na kujadili suala lake na Watford, ambayo inataka pauni milioni 36 kwa ajili ya mshambuliaji huyo.(Mail)

Sarr pia ametambulika na Manchester United kama mbadala ikiwa mpango wa kumnasa winga wa Borussia Dortmund Jadon Sancho utashindwa.(Independent)

Mashetani wekundu pia wanafikiria uhamisho wa winga wa Inter Milan Ivan Perisic, 31, Kingsley Coman,24 anayekipiga Bayern Munich na Douglas Costa kutoka Juventus. (ESPN)

Jadon Sancho alihamia Borussia Dortmund akitokea Manchester City mwaka 2017 kwa kitita cha pauni milioni 10

Manchester United wanamfuatilia kiungo wa kati wa Ujerumani Sami Khedira,33, mkataba wake na Juventus utakapokwisha. (Sun)

Wakala wa Edouard Mendy amedai kuwa makubaliano yameafikiwa kwa ajili ya mlinda mlango huyo, 28, anayekipiga katika klabu ya Rennes kujiunga na Chelsea. (Stades - via Star)

Brentford amekataa ofa ya takriban pauni milioni 10 kutoka Arsenal kwa ajili ya mlinda mlango David Raya, 25. (Telegraph)

Manchester United wanamfuatilia kiungo wa kati wa Ujerumani Sami Khedira

Southampton imeaiambia Tottenham kuwa mshambuliaji Danny Ings,28, hauzwi kwa dau lolote.(Mail)

Leicester City iko karibu kumsajili kwa mkopo mshambuliaji wa Uturuki Cengiz Under,23, kutoka Roma na mlinzi wa Burnley James Tarkowski,27, bado anatolewa macho na Brendan Rodgers.(Sky Sports)

West Ham imebadili muundo wa ofa kwa ajili ya kumnasa Tarkowski lakini ofa hiyo bado imekataliwa na Burnley.(Sky Sports)

Southampton imeaiambia Tottenham kuwa mshambuliaji Danny Ings,28, hauzwi

West Brom wanajaribu kumsajili mshambuliaji wa Aston Villa, Mbwana Samatta, kabla ya mchezaji huyo mwenye miaka 27, hajamaliza mchakato wa kuhamia Fenerbahce. (Sun)

Mlinzi wa zamani wa Liverpool Nathaniel Clyne anafanya mazoezi na klabu ya Crystal Palace na anaweza kupata mkataba na klabu hiyo ya Selhurst Park . (Standard)

Edin Dzeko anajiandaa kujiunga na Juventus akitokea Roma kwa mkataba wa miaka miwili. Uhamisho wa mshambuliaji wa Herzegovina,34, utamaanisha kuwa matumaini ya Luis Suarez kutoka Barcelona huenda yakafikia mwisho.(Goal)

Mbwana Samatta

Arsenal wamekubali masharti ya kiungo wa kati wa Lyon Houssem Aouar, 22. (Star)

Kiungo wa kati wa Tottenhan Dele Alli,24, ameibuka kuwa mlengwa wa Paris St-Germain na Inter Milan. (Mail)

Mshambuliaji wa Serbia Luka Jovic,22, anafikiria kuondoka Real Madrid.(Marca)

Delle Alli anatolewa macho na Paris St-Germain na Inter Milan

Genoa wamefikia makubaliano na Chelsea kumsajili kwa mkopo beki wa kulia wa Chelsea Davide Zappacosta, 28. (DiMarzio - Twitter)

Juventus imethibitisha rasmi uhamisho wa Gonzalo kutoka kwenye klabu hiyo. Mshambuliaji huyo,32, anatarajiwa kujiunga na klabu ya MLS Inter Miami. (Goal)

 

0 comments:

Post a Comment