
Chanzo cha picha, EPA
Baadhi ya wachezaji wa Real Madrid wanadai kuridhishwa na hatua ya kuondoka kwa mshambuliaji wa wa kimataifa wa Wales Gareth Bale kuhamia Tottenham kwa mkopo. (AS - in Spanish)
Rennes wanataka Chelsea kuwajumuisha wachezaji wawili katika mkataba wowowte utakaowahusisha kipa wa kimataifa wa Senegal Edouard Mendy, 28. Beki wa England Fikayo Tomori, 22, ni mmoja wa wachezaji wanaotakiwa na klabu hiyo ya Ufaransa. (Football Insider)
Liverpool imeulizia uwezekano wa kumpata kwa mkopo winga wa Ufaransa na Barcelona Ousmane Dembele, 23. (Sport)

Chanzo cha picha, Reuters
Winga wa Ufaransa na Barcelona Ousmane Dembele
Manchester United wameafikiana na Porto kumhusu beki wao Alex Telles and the 27- sasa kiungo huyo wa kimataifa wa Brazil anaweza kusaini mkataba wa miaka mitano na klabu hiyo. (RMC Sport - via Mirror)
United sasa wanahitaji kufany ahima kukamilisha mchakato wa usajili ili kumpata nyota huyo baada ya Paris St-Germain kujiondoa katika kinyang'anyiro cha kumsaka Telles. (O Jogo - in Portuguese)

Chanzo cha picha, Reuters
Mchezaji wa kimataifa wa Argentina Nicolas Otamendi, 32, kuhamia City
Manchester City wanapania kumsajili beki wa kati na nyuma wa Sevilla Jules Kounde, 21.Hatua hiyo huenda ikamfanya mchezaji wa kimataifa wa Argentina Nicolas Otamendi, 32, kuhamia City. (Telegraph)
Mkufunzi wa Sheffield United Chris Wilder amesema klabu hiyo imefanya mazungumzo na Liverpool kuhusu uhamisho wa mshambuliaji Muingereza Rhian Brewster, 20 kwa mkopo. (Yorkshire Live)

Chanzo cha picha, Huw Evans picture agency
Mshambuliaji Muingereza Rhian Brewster anayesakwa na Crystal Palace
Lakini Crystal Palace pia wanataka kumsajili Brewster kutoka kwa mabingwa hao wa Ligi Kuu ya England kwa mkataba wa kudumu. (90Min)
Leeds bado wana matumaini ya kumsajili kiungo wa kimataifa wa Argentina anayecheza safu ya kati Rodrigo de Paul, 26,kutoka Udinese. (Fabrizio Romano)
Juventus wanataka kumsajili tena Moise Kean, 20, kutoka Everton wakati mshambuliaji huyo wa Italia akijikakamua kutulia Goodison Park tangu alipotua hapo msimu wa joto wa 2019. (Goal)
Pia unaweza kutazama
Matazamo wangu: Ubashiri wa mechi za EPL wikendi hii
Arsenal, Leeds na Wolves wanamfuatilia kiungo wakati wa Reading mwenye umri wa miaka 18 Michael Olise. (Football League World)
Aston Villa wanapigiwa upatu kumsaini winga wa Burkina Faso Bertrand Traore,25,kutoka Lyon. (Sky Sports)
0 comments:
Post a Comment