Paris St-Germain wanavutiwa kumsajili mlinzi wa kati wa Chelsea na Ujerumani Antonio Rudiger, 27, ambapo Chelsea wako tayari kumtoa kwa mkopo na sio kumuuza. (Telegraph - subscription required)

Tottenham wako kwenye mazungumzo na kitasa wa Slovakia ambaye anakipiga kunako klabu ya Inter Milan Milan Skriniar, 25. (Sun)
Inter wanaweza pia kumsajili beki wa kati wa England na Manchester United Chris Smalling 30 kama watashindwa kufikia dau la Mslovakia. (Football Italia)
Sevilla wanatarajia ofa nyingine kubwa kutoka kwa Manchester City inayomhitaji beki wao Jules Kounde, 21. (ESPN)

Chanzo cha picha, Getty Images
Arsenal wametuma ofa ya pauni milioni 32 ya kumhitaji kiungo wa Lyon Houssem Aouar 22 ingawa klabu hiyo inahitaji kiasi cha pauni milioni 54. (RMC Sport, via Metro)
Aouar amekubali kutua The Gunners baada ya klabu aliyokuwa akiihitaji ya Manchester City kutotuma ofa yoyote mpaka sasa. (Telefoot, via Mirror)
Nyota wa Liverpool na England aliye chini ya miaka 20 Rhian Brewster, anavutiwa kutua Sheffield United licha ya klabu ya Aston Villa kuhitaji huduma ya kinda huyo.(ESPN)
Leeds United wanakaribia kumsajili kiungo wa Kiholanzi mwenye miaka 22, Teun Koopmeiners kutokea AZ Alkmaar. (Telegraph - subscription required)

Meneja wa Chelsea Frank Lampard anapanga kufanya mazungumzo na kioa wa Hispania Kepa Arrizabalaga, 25, juu ya hatima yake hasa baada ya kusajiliwa kwa Mendy 28 kutokea Senegal na Rennes.(Star)
Kocha wa Newcastle United Steve Bruce amesema hafikiria kumuuza mshambuliaji wake raia wa Brazil Joelinton, 24, majira haya (Mirror)
Watford wanafikiria kumsajili beki wa kati wa Sheffield United Dominic Iorfa, ambaye amewahi kukitumikia kikosi cha England chini ya miaka 21.(Star).
0 comments:
Post a Comment