Wednesday, September 30, 2020


Jason
Maelezo ya picha,

Sancho alijiunga na Dortumund akitokea Manchester City mwezi Agosti mwaka 2017

Ofa ya Manchester United ya pauni milioni 91.3 kwa ajili ya mshambuliaji wa England Jadon Sancho, 20 imekataliwa na Borussia Dortmund. (Sky Sports)

Na United inahofia kushusha thamani yake ikiwa ofa yake ngingine kwa ajili ya Sancho itakataliwa na Dortmund. (Mail)

Pia wamejiunga na kinyang'anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Real Madrid na Serbia Luka Jovic, 22, kwa mkopo. (AS - in Spanish)

Luka Jovic
Maelezo ya picha,

Luka Jovic

Na inakaribia kufanikiwa kumsajili mshambuliaji wa Barcelona na Ufaransa Ousmane Dembele, 23, - wakiipiga Barca jeki kifedha kumsajili mshambuliaji wa Lyon aliyekuwa Manchester United Memphis Depay. (AS - in Spanish)

Mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich wamewasiliana na Brighton juu ya uwezekano wa makubaliano na beki wa kulia Tariq Lamptey, 19. (Sport1, via Metro)

David Alaba (katikati) ameisaidia Bayern Munich kunyakua mataji manne ya Bundesliga
Maelezo ya picha,

David Alaba (katikati) ameisaidia Bayern Munich kunyakua mataji manne ya Bundesliga

Pep Guardiola anataka kumsajili beki wa kushoto mpya kabla ya dirisha la usajili kufungwa na David Alaba wa Bayern Munich na Austria, pamoja na mchezaji wa Ajax na Argentina Nicolas Tagliafico, wote wakiwa na umri wa miaka 28, wakinyatiwa na Manchester City. (Mail)

Southampton huenda ikachukua hatua ya kuchelewa kumsajili kiungo wa kati wa Heerenveen Uholanzi Joey Veerman. (Voetbal International, via TalkSPORT)

Arsenal's Lucas Torreira was injured in the FA Cup tie at Portsmouth
Maelezo ya picha,

Lucas Torreira wa Arsenal huenda akaondoka klabu hiyo

Ajenti wa Lucas Torreira amefika Madrid kufanya mazungumzo na Atletico Madrid juu ya uwezekano wa kiungo huyo wa kati, 24, raia wa Uruguay kuondoka Arsenal. (Fabrizio Romano, via Express)

Chelsea iko tayari kumuuza mlinzi wa Ujerumani Antonio Rudiger na ingawa Tottenham pia inamkodolea macho mchezaji huyo, 27, ingependelea ikiwa angehamia nchi za nje. (ESPN)

Thiago Silva
Maelezo ya picha,

Thiago Silva aliichezea Paris St-Germain mabigwa wa Ufaransa kwa miaka minane

Beki wa kulia wa Brazil Thiago Silva, 36, anasema "alikasirishwa" na vile Paris St-Germain ilivyoshughulikia kuondoka kwake, na hata ikiwa mabingwa hao wa Ufaransa waliomuongezea mkataba wa mwaka mmoja muda ulikuwa umekwenda kwasababu tayari alikuwa amekubali kujiunga na Chelsea. (ESPN)

Ofa ya West Ham ya mkopo kwa beki wa kulia Vladimir Coufal, 28, wa timu ya Slavia Prague ya Jamhuri ya Czech imekataliwa. (90min)

 

0 comments:

Post a Comment