UONGOZI wa Simba umesema kuwa upo tayari kwa ajili ya mchezo wa ligi dhidi ya JKT Tanzania utakaopigwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma Oktoba 4.
Kesho kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck kinatarajiwa kuanza safari ya kuelekea Dodoma kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo huo.
Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa kila kitu kipo sawa na wanaamini kwamba watakwenda kufanya vizuri kwenye mchezo wao dhidi ya JKT Tanzania.
“Tunakwenda kucheza na JKT Tanzania mchezo wetu utakaochezwa Oktoba 4, ni kazi ngumu tunakwenda kufanya lakini tupo tayari muda wote kupambana ili kuona tunapata ushindi.
"Mashabiki wetu waendelee kutupa sapoti ili kuona namna wachezaji wao wanavyopiga zile pasi sambusa tunajua kwamba kuna ugumu kwenye viwanja vya nje lakini tupo tayari," amesema.
Msimu uliopita wa 2019/20 wakati Simba ikipoteza mechi mbili kati 38 ilizocheza JKT Tanzania ilikuwa ni miongoni mwa iliyoifunga Simba Uwanja wa Uhuru kwa ushindi wa bao 1-0.
0 comments:
Post a Comment