SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuna uwezekano wa kuwatumia nyota wake wawili kesho kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara, Uwanja wa Mkapa.
Simba itakuwa na kazi ya kusaka pointi tatu kwenye mchezo wao wa ligi ambao utakuwa ni wa 12 ndani ya ligi.
Kocha huyo amesema:“Chris Mugalu yupo vizuri baada ya kuwa majeruhi na Joash Onyango amerudi baada ya kupata majeruhi tukiwa Nigeria.
" Kuna uwezekano kesho wakacheza lakini uhakika zaidi ni mchezo ujao wa jumapili," .
Simba ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 23 baada ya kucheza mechi 11 za ligi vinara ni Yanga ambao wana pointi 34 baada ya kucheza mechi 14.
0 comments:
Post a Comment