Tuesday, December 8, 2020


Maradona wa Napoli akiwa na binti yake Dalma mwaka 1989
Maelezo ya picha,

Maradona na binti yake Dalma mwaka 1989

Jalada la mali, haki miliki picha yenye faida, na gari ambalo linaweza kuendeshwa ardhini na majini kutoka Belarus.

Hizi ni baadhi tu ya mali zilizomilikiwa na mwansoka nyota wa zamani wa Argentina Diego Maradona.

Mchezaji huyo raia wa Argentina aliyefariki wiki iliyopita akiwa na umri wa 60, ameacha nyuma hali ngumu lya urithi wa mali yake aliyojikusanyia wakati yeye binafsi akikabiliwa na changamoto za maisha.

Tangu Maradona alipofariki dunia kumekuwa na uvumi mkubwa kuhusu utajiri wake na warithi wanaostahili kupata sehemu ya utajiri huo.

Maradona alikuwa na familia kubwa, akiwa na watoto nane katika miongo kadhaa ya uhusiano wake wa kimapenzi na wanawake sita tofauti. Mali yake inatarajiwa kugawanywa sawa miongoni mwa watoto hao.

Lakini hakuna ripoti kuhusu wosia, huku wataalamu wa kisheria na wa Muargentina huyo na wanahabari wakisema suala la urithi litakuwa tata sana kutatua na huenda usiwe moja kwa moja.

Wanatarajia visa vya makabiliano ya kisheria mahakamani kutatua mzozo wa kifamilia, uchunguzi wa chembechembe za vinasaba DNA na walaghai watakaotafuta njia za kupata urithi wake kwa madai ya kuwa watoto wake huku mawakili waking'ang'ana kuhesabu thamani ya nyumba za Maradona

Maradona na mke wake wa zamani Claudia Villafane (Kushoto) na mabinti zakekatika tamasha la filamu la Cannes mwaka2008
Maelezo ya picha,

Maradona na mke wake wa zamani Claudia Villafane (Kushoto) na mabinti zake

"Naona mchakato wa urithi utakumbwa na mzozo," Elias Kier Joffe, wakili wake aliye na makao yake Buenos Aires, Argentina aliambia BBC. "Huenda ikachukua muda kutatua mzozo huo."

Kwa hivyo, watoto wa Maradona ni wapi?

Kutambuliwa kama baba wa mtoto kupiti auchunguzi wa DNA ilikuwa hali ya kawaida katika maisha ya Maradona.

Mmoja wa mabinti zake wakati mmoja alimtania kwamba anaweza kuunda kikosi cha kwanza cha timu ya mpira ya wachezaji 11.

Kwa miaka kadhaa Maradona alikanusha kuwa na watoto wengine isipokuwa Gianinna, 31, na Dalma, 33, wote wasichana aliozaa na mke wake wa zamani Claudia Villafañe, ambaye alimpatia talaka mwaka 2003 baada ya kuwa katika ndoa kwa karibu miaka 20.

Hatimaye mshindi huyo wa kombe la dunia aliwatambUa watoto sita zaidi kuwa ni wake.

Maradona alizaa mabinti wawili, Dalma na Gianinna, na mke wake wa zamani Claudia Villafañe
Maelezo ya picha,

Maradona alizaa mabinti wawili, Dalma na Gianinna, na mke wake wa zamani Claudia Villafañe

1px transparent line

Maradona aliwatambua Diego Junior, 34, na Jana, 24, kama watoto wake kati kati ya miaka ya -2010 baada ya mzozo wa mahakamani na mama zao ambao aliwahi kuwa katika uhusiano wa kimapenzi nao.

Hakukua na mzozo wa uzazi kumhusu mwanawe wa kiume wa pili aliyezaliwa mwaka 2013,ambaye sasa na miaka saba Diego Fernando.

Maradona na mwanawe wa Diego Junior
Maelezo ya picha,

Maradona alikiri hadharahi kuwa baba ya Diego Junior (Kulia) mwaka 2016

Maradona akiwana binti yake Jana Maradona wakati wa mechi kati ya Boca Juniors na Quilmes mwaka 2015
Maelezo ya picha,

Jana (kulia) alikuwa binti wa tatu wa Maradona baada ya Dalma na Gianinna

Maradona aliwashanaza wengi mwaka 2019, wakati wakili wake aliposema kuwa amekubali kuwa baba wa watoto wengine watatu waliozaliwa Cuba , ambako aliishi miaka kadhaa kutoka mwaka 2000 wakai alipokuwa akifanyiwa matibabu ya kuachana na utumizi wa dawa ya kulevya aina ya cocaine.

Kufikia sasa, kuna karibu watoto wengine wawili zaidi - Waargentina Santiago Lara, 19 na Magalí Gil, 23 - ambao wanaamini Maradona alikuwa baba yao. Wote wanasema watachukua hatua za kisheria kubaini hilo, ambayo watatumia kupigania sehemu ya urithi wa which they will need to Maradona.

A graphic showing Maradona's family tree
1px transparent line

Tayari, wakili wa Bwana Lara ameomba mahakama kumpatia idhini kufukua mwili wa mwanasoka huyo ili kuchukua sampuli ya kufanyia uchunguzi wa DNA. Hata hivyo haijabainika ikiwa Bwana Lara na Bi Gil watabiani kuwa watoto wake, watapokea kiasi gani cha urithi wake.

Urithi unaokadiriwa kuwa wenye thamani ya kati ya $75m (£55m) na $100m ndio ulioangaziwa zaidi na vyombo vya habari vya Agentina. Hii iliangaziwa bili kuashiria chanzo chochote, katika taarifa iliyoandikwa na Julio Chiappetta, mwandishi wa michezo wa Argentina ambaye alikuwa mwandani wa karibu wa Maradona.

Maradona alikadiriwa kuwa na utajiri wa thamani ya $500,000 wakati wa kifo chake, kwa mujibu wa mtandao wa Celebrity Net Worth, unaoripoti Utajiri wa watu maarufu. Tovuti hiyo inasema makadirio ya utajiri unazingatia " uchunganuzi wa kifedha, uchunguzi wa soko, na vyanzo vya ndani".

Thamani ya utajiri wa Maradona inakadiriwa kuwa kiasi gani?

Hakuna ushahidi unaoashiria kiwango cha utajiri wa Maradona, lakini baadhi ya ripoti katika vyombo vya habari zinakadiria kuwa metriki mbili.

Makadirio ya kwanza jumla ya thamani ya mali yote ya Maradona, kutoka kwa magari yake ya michezo hadi vito vyake.

Celebrity Net Worth inasema Maradona alipokea "mamilioni ya dola kutokana na mshahara na ridhaa ya bidhaa" wakati alipokuwa mchezaji na kocha wa mpira .

Sehemu kubwa ya utajiri wake ulitokana na kandarasi ya klabu ya soka ya Italia, Napoli ambako kwa mujibu wa ripoti ya mwaka 1991 Gazeti la New York Times alipokea mshara wa dola milioni tatu ($3m), pamoja na $8m hadi $10m kutoka kwa ridhaa.

A mural of Maradona
Maelezo ya picha,

Mashabiki walimpatia Maradona majina ya utani kama vile "Dios", kumaanisha mungu

Italia ilimjenga na kumsambaratisha Maradona, kumpatia kwa mkono mmoja na kumpokony akwa mkono mwingine. Mwaka 2005, serikali ya Italia ilisema kuwa inamdai Maradona euro milioni 37.2 sawa na dola milioni 48 ya kodi ambayoa haijalipwa kuanzia zama alizokuwa akicheza Napoli.

Hadi wa leo madeni mengi ya nyota huyo wa soka duniani hayajalipwa.

Maradona alikataa kulipa madeni hayo, na kama angelishi miaka mingi zaidi,huenda angeliendelea kufanya hivyo. Hata hivyo ukwepaji wa kulipa ushuru kulisalia kuwa kikwazo kikubwa katika maisha yake.

A fan smiles and hugs Diego Maradona during a party at the Conrad Hotel in 1999 in Punta del Este, Uruguay
Maelezo ya picha,

Maradona alipenda sana kuponda raha

Mmoja wa marafiki zake, mwandishi wa michezo wa Argentina Luis Ventura, alisema mwenendo wa Maradona wa kutumia pesa kiholela ulithiri sana akiba yake. Alipohojiwa katika kipidi cha Televisheni cha Fantino a la tarde, Ventura aliulizwa ikiwa Maradona "alikufa masikini".

"Bila shaka masikini," Ventura alisema. "Alipenda sana kuponda raha, na pia alikuwa mkarimu sana, mtu akimuomba pesa alipampatia bila kinyongo."

2px presentational grey line

Mali yake itagawanywa vipi?

Katika maisha yake yote Maradona amekabiliwa na mzozo unaohusisha wapenzi wake wa zamani na watoto, pande zote zikiweka katika mitandao ya kijamii malalamiko yao au katika Televisheni ya Argentina

Hali ya afya ya Maradona na mali yake imekuwa chanzo cha mizozo. Mwezi November 2019, kwa mfano, Maradona alizungumzia urithi wake baada ya binti yake Gianinna kuelezea hofu yake kuhusu hali ya afya yake katik amitandao ya kijamii.

"Nawaambia nyote kwamba sitaacha kitu changu chocote, Nitatoa sadaka," Maradona alisema katika video iliyowekwa Youtube.

Maradona kisses his daughter Gianinna
Maelezo ya picha,

Maradona na binti yake Gianinna

Baadhi ya mali ya Maradona ambayo aliripotiwa kumiliki ni pamoja na:

  • Karibu nyumba tano nchini Argentina lakini, kulingana na Bwana Joffe alisema, " hana nyumba Beverly Hills "
  • Gari la aina ya Rolls Royce Ghost lenye thamani ya $360,000 na BMW i8 lenye thamani ya karibu $175,000
  • Gari lenye uwezo wa kuendeshwa ardhini na majini alilopewa kama zawadi wakati alipozuru Belarus
  • Pete ya almasi ya thamani ya dola 360,000
  • Kandarasi ambayo inaruhusu Komani kutumia sura ya Maradona kwenye mchezo wa video wa Pro Evolution Soccer
Maradona riding an all-terrain vehicle in Belarus
Maelezo ya picha,

Maradona akiwa ndani ya gari ambalo linaweza kuendeshwa popote ardhini na majini zawadi aliyopewa alipozuru Belarus mwaka 2018

Chini ya sheria ya Argentina, hatahivyo mtu anaweza kupeana thuluthi moja ya mali yake, na sehemu inayobakia kupewa mke na watoto

Kwa kuwa Maradona huenda hakuacha wosia, na hakuwa na mke wakati wa kifo chake, watoto wake ndi wanastahili kugawanyiwa mali yake yote kwa usawa.

"Waargentina hawana utamaduni wa kuandika wosia. Watu wengi hawafanyi hivyo," Bwana Joffe alisema.

BBC iliwasiliana na wakili wa Maradona, Matías Morla, kumuuliza kuhusi wosia wake na masuala mengine, lakini hadi taarifa hii inachapishwa, haijapokea majibu.

Bila wosia mambo yatakuwa magumu.

2px presentational grey line

Maelezo zaidi kumhusu Diego Maradona:

 

0 comments:

Post a Comment