Tuesday, December 8, 2020

 


Kiungo wa kati wa Arsenal Mesut Ozil, 32, ana uhakika wa 90% wana uhakika atajiunga na Fenerbahce

Kiungo wa kati wa Arsenal Mesut Ozil, 32, ana uhakika wa 90% wana uhakika atajiunga na Fenerbahce mwezi ujao, kwa mujibu wa mmoja wa wajumbe wa bodi ya Fenerbahce .(Sport Digitale, via Mirror)

Wawakilishi wa Jesse Lingard wanapitia ofa za mkopo kwa kiungo huyo wa Manchester United na England mnamo Januari, na Real Sociedad moja ya vilabu ambavyo wamefanya mazungumzo ya awali nae kuhusu mchezaji huyo mwenye miaka 27. (Sky Sports )

Kocha wa Chelsea Frank Lampard amesema hana shinikizo la kumuuza mlinda mlango wa Uhispania Kepa Arrizabalaga, 26, mwenye thamani ya pauni milioni 71,(Evening Standard)

Wawakilishi wa Jesse Lingard wanapitia ofa za mkopo kwa kiungo huyo wa Manchester United na England mnamo Januari

Kocha wa Chelsea Frank Lampard amesema hana shinikizo la kumuuza mlinda mlango wa Uhispania Kepa Arrizabalaga, 26, mwenye thamani ya pauni milioni 71,(Evening Standard)

Manchester United inaweza kumgeukia mlinzi wa pembeni wa Real Madrid ya Uhispania, Lucas Vazquez, 29, wakati wanatafuta mshindani wa Mwingereza Aaron Wan-Bissaka, 23.(Defensa Central - in Spanish)

Manchester United wana nia ya kumruhusu mlinda mlango wa Argentina Sergio Romero kuondoka mwezi ujao na watamuuza ikiwa dau la pauni milioni 2 litafikiwa.(Football Insider)

Kocha wa Chelsea Frank Lampard amesema hana shinikizo la kumuuza mlinda mlango wa Uhispania Kepa Arrizabalaga

Mshambuliaji wa Brazili Hulk, 34, ameondoka Shanghai SIPG na amehusishwa na taarifa za kuhamia ligi ya primia kwa uhamisho huru.(Sun)

Tottenham na Arsenal waelezwa kumtaka kiungo wa kati wa AC Milan na Ivory Coast, Franck Kessie, 23, ambaye ana thamani ya karibu pauni milioni 45 na ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mnamo Juni 2022. (Calciomercato - kwa Kiitaliano)

Liverpool ina matumaini ya kuanza mazungumzo na kiungo mkabaji Faninho, 27, kuhusu mkataba mpya hivi karibuni.(Guardian)

Liverpool ina matumaini ya kuanza mazungumzo na kiungo mkabaji Faninho

Mholanzi Jetro Willems amekataa ofa ya mkataba mpya katika klabu ya Eintracht Frankfurt, hatua inayotoa fursa kwa Newcastle kumsajili mlinzi huyo, ambaye alikuwa akichezea Magpies kwa mkopo msimu uliopita. (Chronicle)

Newcastle wanalenga kurudi katika kambi yao ya Benton Jumanne huku wakitafuta kuendelea na mazoezi baada ya ugonjwa wa Covid-19 kusababisha kuahirishwa kwa mechi yao na Aston Villa. Magpies wanatumai mechi yao na West Brom itafanyika kama ilivyopangwa mwishoni mwa wiki hii.(Chronicle)

1 comments:

  1. Best Real Money Casino Apps in USA 2021 - CasinoWow
    Slots Casino — One of the 1xbet 먹튀 most jancasino.com recognizable online slots games around. This game's most recent is the Playtech 🏆 Best Real Money Casino 1등 사이트 App: SlotWolf🎁 #1 USA Casino Bonus: apr casino Risk Free Spins for $1,000🏆 Best Real Money Casino App: SlotsMillion

    ReplyDelete