Tuesday, September 28, 2021

 


MABINGWA watetezi, Simba SC wamelazimishwa sare ya bila kufungana na wenyeji, Biashara United katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Karume, Musoma mkoani Mara.
Nahodha na mshambuliaji tegemeo, John Raphael Bocco  hatalala vizuri leo baada ya kuikosesha ushindi timu yake kufuatia mkwaju wake wa penalti kupanguliwa na kipa Mganda, Cleo James Ssetuba dakika ya 90.
Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, bao pekee la Cleophace Mkandala dakika ya 33 limewapa wenyeji, Dodoma Jiji FC ushindi wa 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
Na Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya, bao la Peter Mapunda dakika ya 90 na ushei limeipa Mbeya City ushindi wa 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons.

0 comments:

Post a Comment