Tuesday, September 28, 2021



 COASTAL Union ya pale Tanga Mji Mkongwe, leo imepindua meza dakika za lala salama kwenye mchezo wake wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Azam FC iliyosafiri umbali wakutosha kutoka Dar es Salaam.

Ni kwenye mchezo wa ligi ambao ni wa kwanza kwa timu zote mbili msimu mpya wa 2021/22 ambao umeanza leo Septemba 27.

Baada ya dakika 90, ubao wa Uwanja wa Mkwakwani ulisoma Coastal Union 1-1 Azam FC na kuwafanya wagawane pointi mojamoja.'

Walikuwa Azam FC walianza kupachika bao la kuongoza dakika ya 82 kupitia kwa Amoah ambaye alifunga bao hilo kwa kichwa akiwa ndani ya 18 kilichomshinda kipa namba moja Mussa Mbissa.

Ikiwa zimebaki dakika 8 mchezo huo kukamilika, Coastal Union waliweka usawa dakika ya 89 kupitia kwa nyota wao Hance Masoud ambaye naye alifunga bao hilo kwa kichwa.

Akizungumza na Saleh Jembe, Masoud amesema kuwa ni jambo la kushukuru kwa Mungu kwa kupata pointi moja kwa kuwa mchezo ulikuwa ni mgumu.


0 comments:

Post a Comment